Na Godson Mbilinyi
Dar Kugumu ila amekomaa na sasa Dar kwake ni rahisi kila anapogusa panaitika, kama utani Baba wa mtoto mmoja tena aliyezaa na mtoto wa masuper staa aseme nini zaidi ya kusema Asante kama kwenye wimbo wake. Tuachane na hayo hapa tuzungumze kilichotukusanya jana pale Coco Tips Dar es Salaam kwa Baba Huyu ambaye bado ni Toto Bad malizia basi au bado basi wacha nimalize Marioo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_0998c8728d9c4565aa775206372b763e~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_0998c8728d9c4565aa775206372b763e~mv2.jpeg)
Nilitamani nichambue nyimbo lakini sikio langu bado halijatosheka limeonja utamu kidogo kama ilivyo kwa wengi na kubaini kwamba hadi sasa ngoma ya Wangu akiwa na Harmonize kama imepenya haraka katika mpya zilizopo ndani albamu hii ya Wajina "The Godson" usishangae wajina nami mwandishi wako jina langu ni Godson, ipo hivi naomba nizungumze juu ya mtiririko wa tukio.
Sio mbaya penye maua tutoe maua kwenye sindano tupige sindao, tukianza kwenye mpangilio wa kutangaza tukio Marioo hapa Menejimenti twawapa maua kadhaa tu ambayo ni ya machapisho ya kutangaza tukio kwenye rangi, graphics na maudhui kwa ujumla yalivutia alitoa maelezo muhimu juu ya kila taifa alilolishirikisha kwenye albamu, alialika watu wa kada tofauti tofauti za Burudani ila ndugu zetu wa Bongo Movie aliwatenga wakati ujao usicheze nao mbali.
Tuje mpangilio wa tukio upande wa entrance haikuwa ya mvuto sana kiasi kwamba ilikuwa finyu kiasi hata cha wageni wanaoingia kubughudhiwa na pilika pilika za watu, uchaguzi wa location ni kama haukuwa mtamu sana eneo dogo kiasi cha idadi ya watu kuwa kubwa na kufanya washindwe kujinafasi, pongezi kwa MC wa jambo Adam Mchomvu alifanya vyema alijua kushirikiana na wana habari kwa kila tukio.
Upande wa Dressing Code waalikwa walijitahidi kufuata maelekezo White ilitawala ingawa Marioo hakuwa kivile. Paula na Marioo walijitahidi kwenda na muda ingawa wakati ujao waboreshe zaidi.
Upande wa decoration haukuwa poa sana kuanzia stage n.k hapo kwenye stage watu walijazana bila sababu za msingi muda wote kiasi cha kumnyima nafasi mwenye tukio kujinafasi vizuri. Tukio la Marioo uzinduzi wa albamu iliyopita The Kid You Know lilifana sana tulitegemea mwaka huu ifunike zaidi lakini haijawa hivyo next time iboreshwe zaidi.
Wewe je umeikubali ngoma gani?
Comments