top of page
Radio on air

JITAHIDI UWE HAMASA - SHILOLE

Kutoka kwa mwanadada Shilole ambaye ni msanii na Mjasiriamali amefunguka ujumbe huu

"Kwa Wadogo zangu, na Watoto wangu, Nani aliwadanganya kuwa na makalio makubwa ndio



kufanikiwa? Nani aliwadanganya kufanya mambo ambayo hayampendezi maulana ndio kufanikiwa?

Wakati natoa #NakomaNaJiji mengi yalikuwa yakizungumzwa, Wengi walisema nirudi kwetu Igunga kwasababu huu mji nimeushindwa, Nilichoimba kwa wakati huo ulikuwa ni ukweli mtupu ilifika kipindi nilikuwa ninazungumza na Mungu wangu tu, Yatima mimi ambaye kutafuta sijachoka, Mungu alinijalia sikuweza kuanguka.

Nani aliamini kwa kipindi kile nitaweza kufungua migahawa ya chakula mkubwa na kufanya vizuri kila kona. Jiulize ni watu wangapi maarufu walianzisha biashara na wakashindwa kusimamia? Tazama @shishifood na ujifunze.

Somo langu kubwa kwa wadogo zangu na watoto wangu, Hii dunia imejaa kila aina ya watu jitahidi uwe moja kati ya watu wema, Jitahidi uwe hadithi nzuri siku ukiondoka : Mimi ni hamasa kwa kundi kubwa la Wanawake wenye ndoto wale wanaopitia magumu sana, Wale wanaotoka hali ya chini sana." @officialshilole

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page