top of page

JOTI NA MKEWE WATIMIZA MIAKA 7 YA NDOA YAO "HATA NIKIWA SINA HELA NAKUTA UMEPIKA KUKU"

Mchekeshaji maarufu Joti ameweka wazi kutimiza miaka saba ya ndoa yake ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka ujumbe huu maridhawa


"ASANTE SANA MUNGU WETU.

Happy 7th Anniversary for Us.


Tunaendelea kukushukuru Mungu Mkuu kwa namna Unavyotupigania Mimi na huyu Mnyakyusa wangu.. Sasa tumefikisha Miaka 7 ya Ndoa Yetu ni nani wakutukuzwa kama sio wewe MUNGU..


Sala, Maombi, Kutafuta, Kushukuru ndio Nguzo kwetu.. Asante MUNGU kwa kunipa huyu Mwanamke.. Na kama Unavyojua kuna kipindi mimi mwanaume ninapenda sana Utulivu pindi ninapokosa Pesa au Kuzitafuta, lakini kwa huyu Mama Junior/Mama twins hapana jamani Unanipa faraja sana.. Uniombi hela Mara kwa mara..6000


Nikiwa sina hela Usiku nakuta umepika Kuku..

Sasa sijui pesa Unatoa wapi? Au ndio zile zangu ninazokupa

Ikn huwa unazichimbia, Mwanamke unajua mahesabu wewe Nakupenda wewe na watoto wangu.. Mungu akatusimamie Tuzeeke Pamoja tukiwa hatuna hata Meno."

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page