top of page

KAMA TULIVYOGUSWA NA TAARIFA YA FIFA TUGUSWE NA KULIPIA ADA ZETU -KAMWE

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Meneja habari na mawasiliano Yanga SC Ally Kamwe amefunguka haya

"Leo, Nimepokea simu na meseji nyingi kutoka kwa Mashabiki wakiuliza kuhusu Taarifa ya Klabu yetu ya @yangasc Kufungiwa Kusajili na FIFA.

Ni Taarifa iliyogusa Hisia za Wanayanga wengi mno kiasi cha kila mtu kutamani kujua ukweli wa Jambo hili... Na hapa nikaona kuna ulazima wa kusema machache

Kwanza, Ni Taarifa ya kweli na Tayari Uongozi wetu umeshachukua Hatua za kulimaliza Jambo hili. Ni Fedha za awamu ya mwisho ambazo kwa mujibu wa makubaliano, Tunapaswa kuzilipa



kama ambavyo Tulishalipa awamu zilizopita kwa Mchezaji Kambole.

Lipi neno langu kwa Mashabiki wa @yangasc?

Kama na wewe ni sehemu ya watu walioguswa na Taarifa hii na mpaka sasa Hujalipia Kadi yako ya Uwanachama, Basi Tambua wewe ndio Unashiriki kwa Asilimia kubwa kuirudisha nyuma Klabu yako.

Mudq huu Tunapoketi kwenye vijiwe vya Soka na kujivunia/ Kutamba kuhusu Ubora wa Klabu Yetu Ni Lazima Tutambue KUNA KAZI KUBWA INAFANYIKA kuiweka @yangasc Yetu kwenye Levo hizo.

Viongozi wanaumiza sana vichwa kuhakikisha wanabuni vyanzo mbalimbali vya kuongeza Pato la klabu yetu na kumsaidia Bosi wetu GSM katika kuipeleka Klabu yetu kwenye Nchi ya ahadi

Niwaombe, Tuwasaidie VIONGOZI WETU.

Sisi Wanachama Jukumu letu kubwa kwa sasa ni KULIPA ADA zetu kila Mwaka. Hili ni MUHIMU mno na Ndio linapaswa kutuumiza mno pale unapomuona Mwananchi mwenzako akiwa anavimba na @yangasc na Hajalipia Ada yake ya Uwanachama

Kama Tulivyoguswa na Taarifa ya FIFA leo.. Tuguswe pia na KUHAMASISHANA wenyewe kwa wenyewe Kulipia Ada zetu. Furaha ya mpira ni GHARAMA

Sisi tuna Furaha sana.. Kuifanya Furaha yetu idumu ni lazimq Tukubali kuigharamia.

LIPA ADA YAKO MWANANCHI.. TUIJENGE PAMOJA YANGA TISHIO AFRIKA" Ally Kamwe

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page