Na VENANCE JOHN
Kamanda mkuu wa kundi la dola la kiislamu (ISIS), Shirwac Aw-Saciid nchini Somalia amekamatwa. Taarifa hizi zimeripotiwa na polisi na vyombo vya habari vya serikali, huku vikosi vya usalama vikiendelea na mashambulizi ya wiki moja dhidi ya kundi hilo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_acfbb2bc76584218a082f3d2952c405a~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_acfbb2bc76584218a082f3d2952c405a~mv2.jpeg)
Abdirahman Shirwac Aw-Saciid, mkuu wa kikosi cha mauaji ya kundi hilo, alijisalimisha kwa mamlaka hapo jana katika milima ya Cal Miskaad, kaskazini mashariki mwa jimbo la Puntland. Kushikiliwa kwa kamanda huyo kumekuja siku mbili baada ya uongozi wa ISIL nchini humo kulengwa na mashambulizi ya anga ya Marekani.
Katika miaka michache iliyopita, tawi la ISIL la Somalia limekuwa sehemu muhimu zaidi ya mtandao wa kundi hilo duniani kote, likiongezeka kwa nguvu kwa sababu ya kufurika kwa wapiganaji wa kigeni na kuboreshwa kwa ukusanyaji wa mapato.
Jana Jumatatu, mkuu wa polisi katika mkoa wa Bari wa Puntland, Abdikadir Jama Dirir, alithibitisha kukamatwa kwa Aw-Saciid, anayejulikana kwa jina la "Laahoor", ambaye pia alikuwa akihusika na unyang'anyi wa biashara za ndani kwa kundi hilo. Eneo la kaskazini mashariki mwa Somalia la Puntland lilitangaza mashambulizi makubwa dhidi ya ISIL na kundi pinzani, la al-Shabab lenye mafungamano na al-Qaeda, mwezi Disemba.
コメント