top of page

KAMBI MAALUMU YA UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO YATUA WILAYANI NAMTUMBO...

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam Kwa ushirika mkubwa kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la



namtumbo Mhe. Vita Rashid Kawawa Kutoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo, vipimo vya Echo na ECG kwa wananchi.

Huduma zote zitatolewa Bure Kwa wananchi wa Wilaya ya Namtumbo katika Viunga vya Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo (migelegele) Julai 8 hadi 9 2024, Kituo cha Afya cha Lusewa Julai 11 hadi 12 2024 na Kituo cha Afya cha Mputa Julai 13 hadi 14 2024 Upimaji huu ufanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia saa Moja kamili asubuhi hadi saa 12 kamili jioni.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page