Na VENANCE JOHN
Kampuni ya utafiti kutoka Marekani ambayo ilikuwa imechapisha ripoti zinazoshutumu mashirika makubwa ya kifedha nchini India na nje ya nchi kwa makosa ya kifedha na ulaghai inatazamiwa kufungwa. Nate Anderson, mwanzilishi wa kampuni ya kufanya Utafiti ya Hindenburg, ametangaza jana Jumatano kwamba alikuwa akiivunja kampuni hiyo karibu miaka minane baada ya kuianzisha.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_ecb18b3cbd6141e9b61b8551a590027a~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_ecb18b3cbd6141e9b61b8551a590027a~mv2.jpeg)
Mwaka jana, Utafiti wa Hindenburg ulimshutumu Madhabi Puri Buch - mkuu wa mdhibiti wa soko la Securities and Exchange Board of India (Sebi) - kuwa na uhusiano na fedha za nje ya nchi zinazotumiwa na kampuni ya Adani.
Kampuni hiyo ilikuwa imegonga vichwa vya habari nchini India mwaka wa 2023 baada ya kuchapisha ripoti kuhusu muungano wa bilionea Gautam Adani, na hivyo kuzua mizozo ya kisiasa na hasara kubwa kwa kampuni hiyo. Bwana Anderson hakutoa sababu maalum ya uamuzi wake wa kutaka kufunga kampuni yake ya utafiti.
Hindenburg ilianzishwa mwaka wa 2017, na Utafiti wa Hindenburg ulijipatia umaarufu kwa kufichua madai ya hitilafu za kifedha katika baadhi ya biashara zenye majina makubwa. Ripoti za kampuni hiyo zimesababisha biashara, nchini India na nje ya nchi, kupoteza mabilioni ya dola katika thamani ya soko.
"Takriban watu 100 wameshtakiwa kiraia au kwa uhalifu kama sehemu ya kazi Hindenburg, ikiwa ni pamoja na mabilionea. Mwaka 2020, kampuni hiyo ilishutumu kampuni ya kutengeneza malori ya umeme ya Nikola Corp kwa kupotosha wawekezaji kuhusu teknolojia yake.
Comentários