Mpekuzi anasema kumekuwa na tabia za baadhi ya kampuni za Mapishi/Vyakula (Catering) kupunja watu wanaowahudumia chakula kwenye tender walizopewa wakati mwingine kuficha hasa vyakula kama Nyama jambo linalofanya watu wengi walalamike.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_15db801d4ed0457d8d810446d9156d02~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_15db801d4ed0457d8d810446d9156d02~mv2.jpg)
Mpekuzi anasema ameshashuhudia baadhi ya Sherehe anaona nyama zile pale ila wahudumu wanakatazwa kutoa na kiongozi wao au wenyewe tu wanakuwa wakisema zimeisha ilihali anaziona zile pale.
Mpekuzi anajiuliza kwani kile chakula wanapeleka wapi? Si wamelipwa kwa ajili ya tender hiyo sasa inakuaje wafiche vyakula vingine?
Kwako mdau watu umewahi kukutana na kadhia hii?
Comments