top of page

KAULI HIYO SIYO MSIMAMO WA JESHI LA POLISI

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi kwa umma inaeleza kuwa


"Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema "RPC: ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.





Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo) ni, Je, upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.


Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi na kwamba kauli sahihi ya Jeshi la Polisi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4, 6 na 9, 2024. Vile vile, tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa wa kesi hiyo watafikishwa mahakamani leo Agosti 19, 2024. Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake.


Aidha, wakati uchunguzi wa kupata usahihi wa kauli hizo ukiendelea, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi."

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page