top of page

KESI YA RAIS WA CHAMA CHA SOKA HISPANIA KUMBUSU MCHEZAJI BAADA YA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA YAANZA

Na VENANCE JOHN


Mshindi wa Kombe la Dunia la Wanawake wa Hispania Jenni Hermoso amekabiliana na bosi wa zamani wa shirikisho la soka Luis Rubiales siku ya leo katika kesi yake, akisema hakubaliani na busu ambalo lilizua upinzani na ukosoaji wa kitaifa dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia katika michezo.


Hii ni kuhusu tukio lililoonekana moja kwa moja kwa mamilioni ya watu duniani kote kwenye sherehe za utoaji tuzo za Kombe la Dunia kwa wanawake la 2023 nchini Australia. Jenni Hermoso ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Hispania ya wanawake mwenye umri wa miaka 34.


Luis Rubiales ambaye ana umiri wa miaka 47 kwa wakati huo alikuwa rais wa shirikisho la mpira nchini Hispania, na anatuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na kisha kujaribu kumshurutisha Hermoso kwa usaidizi wa wanaume wengine watatu kwa kutangaza kwamba busu hilo lilikuwa la makubaliano. Ingawa aliomba radhi, Rubiales anakanusha mashtaka hayo ya unyanyasaji wa kijinsia.


Alipoulizwa na mwendesha mashtaka katika Mahakama Kuu ya Madrid ikiwa alikubali busu hilo, Hermoso alijibu; "Kamwe". Kashfa hiyo ya busu ilichukua mijadala mingi sana katika vyombo vya habari ndani na nje ya Hispania.


Rubiales na washtakiwa wenzake, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake Jorge Vilda, mkurugenzi wa zamani wa michezo wa shirikisho la soka la Uhispania (RFEF) Albert Luque na mkuu wa zamani wa masoko wa RFEF Ruben Rivera watatoa ushahidi wao Februari 12 baada ya mahakama kuwahoji mashahidi wengine.


Upande wa mashtaka unatafuta kifungo cha miaka 2-1/2 kwa Rubiales, ingawa nchini Hispania wale wanaohukumiwa chini ya miaka miwili wanaweza kukwepa kifungo kwa kulipa fidia kama mbadala lakini ikiwa hawana hatia ya awali.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page