top of page

KIFAA CHA KUPANDIKIZA KWENYE UBONGO KUTIBU TATIZO LA KUSAHAU, MBIONI KUKAMILIKA

Na Ester Madeghe,


Watafiti nchini Uingereza wamepewa fursa za kufanya majaribio ya kuleta matokeo ya kutibu watu wanaougua shida ya akili, unyogovu na maumivu sugu. Vifaa vinavyoweza kupandikizwa kwenye ubongo vinaweza kugundua shughuli isiyo ya kawaida kwa kufuatilia ubongo kila mara na kurekebisha kwa upole inapohitajika.


Matokeo ya utafiti uliochapishwa na wanasayansi wa Marekani mwaka 2021 yalikuwa na matumaini kwamba suluhu inaweza kupatikana kwa kupandikiza vifaa vya kuingiza kwenye ubongo ili kutibu uchovu mkubwa wa kiakili.


Profesa George Mellieras, mmoja wa wanasayansi wakuu kwenye timu ya chuo kikuu cha Cambridge, anatumai hilo litasaidia kuleta matokeo katika jaribio hilo. Sasa, timu ya Cambridge kutoka sekta ya afya, sayansi na biashara imepewa ufadhili wa mamilioni ya dola kugundua kwa haraka teknolojia mpya zinazolenga kuboresha afya ya ubongo.


Chuo Kikuu cha Cambridge kinakadiria kuwa na baadhi ya watu wenye matatizo ya neva na matatizo ya kiakili ambayo huwaathiri watu wanne kati ya watano, ambapo timu hiyo inatafiti vifaa vidogo ambavyo vinaweza kuwasaidia kutoa matibabu. “Vipandikizi vya Ubongo vinaweza kutoa tiba mpya ya magonjwa ambayo hayawezi kutibiwa kwa dawa,” anaeleza Profesa Melliaras.


Profesa Melliaras." Anasema Elektrodi zinazotoka kwenye kifaa hicho hazipaswi kuwa kubwa kuliko neuroni moja ambapo ukubwa huu ni mdogo mara tano kuliko kipenyo cha nywele za binadamu". Vipandikizi vya matibabu si vipya kwa wahandisi hawa kwani Dk. Chaukun Tong anatengeneza kifaa ambacho hufunika mishipa dhaifu ya binadamu bila kuiharibu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page