top of page
Radio on air

KIHONGOSI ATEULIWA KUWA MKUUWA MKOA WA SIMIYU, RC NAWANDA UTEUZI WAKE UMETENGULIWA...

Taarifa iliyotufikia mezani hivi punde Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi kama ifuatavyo:




1. Amemteua Bw. Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi, Bw. Kihongosi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Bw. Kihongosi anachukua nafasi ya Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

2. Amemteua Bw. Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Kabla ya uteuzi, Bw. Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

3. Amemteua Bw. Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Bw. Magala anachukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

4. Amemteua Bw. George Hillary Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi, Bw. Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Uapisho wa Mkuu wa Mkoa na Msajili wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page