top of page

KIINGILIO NI BUKU TU MECHI YA KUKABIDHIWA UBINGWA KWA MKAPA SUPU YA UBINGWA KAMA KAWAIDA IPO...

Kutoka kwa Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amefunguka haya

"Mchezo wa tarehe 25 Mei 2024 dhidi ya Tabora United, Young Africans SC tutakabidhiwa Ubingwa wetu na wadhamini wetu NBC, mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Mkapa.

Siku nzima Wananchi tunapaswa kutamba na kuvimba, mageti yatafunguliwa saa tano asubuhi. Kutakuwepo na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa kuanzia saa tano" @alikamwe

"Kwenye mechi ya kukabidhiwa Ubingwa dhidi ya Tabora tutakuwa na jambo kubwa na la kihistoria kwenye mechi za kukabidhiwa Ubingwa katika nchi hii. Mwananchi ukikosa hii



surprise ya kipekee basi ujilaumu wewe mwenyewe. Popote ulipo anza safari uje kwenye Jumamosi ya Kibingwa.

Siku ya kukabidhiwa Ubingwa tutakuwa na MaDJ watakaokuwepo. Kuanzia leo tutaanza kutaja orodha ya MaDJ watakaotupatia burudani ya Ubingwa akiwemo DJ Ally B. Tutataja na wasanii wakubwa ambao tutawashusha kwa Mkapa" @alikamwe

Viingilio vya chini katika mchezo huo itakuwa ni Tsh 1,000 katika eneo la mzunguko huku VIP C ikiwa ni Tsh 5,000 na VIP B ni 10,000 huku VIP A zote tayari zimekwisha.

Aidha Parade la Ubingwa litakuwa tarehe 26 hii ikiwa ni mkesha wa kutoka tarehe 25 hivyo wataamkia pale pale kwa Mkapa hivyo Parade litaanzia kutoka hapo uwanjani hadi makao makuu ya Young Africans SC Jangwani Kariakoo Dar es Salaam Tanzania ambapo kabla ya Parade wananchi watapata supu kwanza saa 2 asubuhi.

"Mnamo tarehe 26 Mei 2024 tutakuwa na PARADE LA UBINGWA, Tutaanzia Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia asubuhi kuja Jangwani. Najua miongoni mwa vituo vyetu mnavijua... Safari hii hatupiti tu, tutakaa hapo kwa muda.

Kabla ya PARADE la Ubingwa siku ya Jumapili (25 Mei) tunatarajia kuwa na Supu Day ya kusherehekea Ubingwa hapo hapo Lupaso. Tumeshapata ahadi ya ng'ombe sio chini ya 8 hadi hivi sasa. @alikamwe

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page