Hatimaye Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally ameibuka na kuzungumza juu ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga SC waliopoteza kwa kufungwa bao moja sifuri kwenye Ligi Kuu ya NBC ambapo ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram. "Tunaumia kwa kupoteza mchezo wa derby lakini tunajipongeza kwa kuwa mradi wetu wa kutengeneza timu umeanza kutoa matunda tena kwa haraka sana
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_ab9ff46ec1544422a681c49803a6e741~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_ab9ff46ec1544422a681c49803a6e741~mv2.jpeg)
Wote ni mashahidi misimu kadhaa nyuma tulifungwa derby na kutawalia na mpinzani kwa dakika zote 90. Jana tumeona tofauti kubwa sana tumefungwa lakini tumeutawala mchezo kwa asilimia kubwa na kama kila kitu kingekua sawa basi tungeshinda mchezo ule
Muhimu kwetu Wana Simba kwanza tukubali tumepoteza na wala hakuja haja ya kuanza kuhesabu tumepoteza mara ngapi, Mpira ni maisha ya duara muda wetu utafika na sisi tutatawala derby kwani tumewahi kufanya hivyo
Muhimu kwa sasa ni kusahau yote yaliyotokea na kujipanga upya kwa vita iliyo mbele yetu. Tumebakiwa na michezo 24 nguvu kubwa iwe kushinda michezo hiyo tumepoteza derby sio ubingwa Na pia tuwekeze nguvu kwenye mchezo wetu Jumanne dhidi ya Tanzania Prison
Ubaya Ubwela unaendelea."
Comments