top of page

KIONGOZI WA KIJESHI ANAYEPANGA MASHAMBULIZI UKRAINE AUAWA KWA BOMU JIJINI MOSCOW

Na VENANCE JOHN


Kiongozi wa kundi la kijeshi wanaoiunga mkono Urusi kutoka mashariki mwa Ukraine, Armen Sarkisyan, ameuawa leo na wengine watatu kujeruhiwa wakati bomu lilipolipuka katika sehemu za jengo la kifahari mjini Moscow. Taarifa hizi zimeripotiwa na vyombo vya habari vya Urusi, likiwamo shirika la habari la serikali TASS. TASS iliita shambulio hilo kuwa ni mauaji yaliyopangwa vizuri.


Bomu hilo limelipuka wakati Sarkisyan, akifuatana na walinzi wake, wakiingia chini ya jengo la "Scarlet Sails" kwenye ukingo wa Mto Moskva kilomita 12 tu kutoka Ikulu ya Kremlin. "Jaribio la kumuua Sarkisyan lilipangwa kwa uangalifu na kuamriwa. Wachunguzi kwa sasa wanatambua wale walioamuru uhalifu huo," TASS ilimnukuu afisa mmoja wa Urusi akisema.


Ikumbukwe kuwa mwezi Desemba, 2024, huduma ya usalama ya SBU ya Ukraine ilimtaja Sarkisyan kama bosi wa uhalifu katika eneo la Donetsk, ambalo sehemu kubwa yake imekuwa ikidhibitiwa na Urusi tangu 2014, na kusema kwamba alishukiwa kwa kushiriki na kusaidia makundi haramu yenye silaha.


Taarifa zilizeleza kuwa Sarkisyan alikuwa ameunda kitengo cha kijeshi kinachounga mkono Urusi kilichoundwa na wapiganaji wa ndani ya Ukraine na alikuwa amepanga ununuzi wa vifaa kwa wanajeshi walio mstari wa mbele katika mapigano.

Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page