Na VENANCE JOHN
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Msumbiji Venâncio Mondlane amesema kuwa yuko tayari kuhudumu katika serikali ikiwa Rais wa sasa Daniel Chapo atatimiza matakwa yake ya kumaliza mzozo wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_84f5284feecb4f21a0f31ab4dac446de~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_84f5284feecb4f21a0f31ab4dac446de~mv2.jpeg)
Machafuko ya kisiasa nchini Msumbiji yamtokea baada ya uchaguzi mkuu kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata. Chapo alisema ameunda timu ambayo inazingatia iwapo mpinzani wake anafaa kualikwa kujiunga na serikali mpya ambayo jumuishi.
Mondlane alikataa kushindwa kwake katika uchaguzi wa Oktoba, akisema matokeo yalikuw na udanganyifu jambo ambalo Chapo mara zote amekuwa akikanusha. Mahakama ya juu zaidi ya Msumbiji ilimtangaza Chapo kuwa mshindi kwa kupata asilimia 65 ya kura dhidi ya 24 za Mondlane.
Chapo alikuwa mgombea wa chama tawala cha FRELIMO, kwani mtangulizi wake, Filipe Nyusi, aling’atuka baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Maandamano ya baada ya uchaguzi ya Msumbiji yanaendelea huku kukiwa na wito wa mazungumzo
Comments