top of page

KIPAJI CHA LAIZER KINAAMUA NDOTO KUBWA - BABUTALE

Wakati mjadala ukiendelea mitandaoni juu ya Mtayarishaji gani wa muziki ni mkali Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale maarufu kama Babutale ameibuka na kumpa maua haya mtayarishaji Ayo Lizer ambapo ameandika ujumbe huu

"KIPAJI CHA LAIZER KINAAMUA NDOTO KUBWA.

Leo nimesikiliza sana kazi za miziki inayotamba kwa kiasi kikubwa hapa nchini, basi kila ninaposikiliza mpaka mwisho wa wimbo nasikia jina la huyu kijana @lizerclassic

Hapo ndio nimebaini kuwa kuna SHABIKI WA MUZIKI na kuna SIKIO LA MUZIKI.

Kijana huyu analo sikio la muziki kiasi cha kwamba asilimia kubwa ya Wasanii nchini wanapomaliza kurekodi nyimbo zao, huwa awawezi kuzitoa mpaka @lizerclassic apitishe SIKIO lake kwenye hiyo kazi.




Kwa kifupi huyu ndiye Mtayarishaji wa Muziki (Producer) anayefanya walaji wa muziki tusikie nyimbo nzuri zilizotulia na kukidhi hitaji la ngoma za madikio yetu, mwili na ubongo pia.

Mimi najua kwenye ugawaji wa milabaha inayotokana na kazi za Wasanii anakipande chake kwenye kila nyimbo anayoigusa, na watu wa aina hii kufa njaa ni ngumu sana, hivyo kwenye zile heshima zisizo na kificho wala kupangwa wewe ni Real (GOAT) kwenye hiki kizazi cha waandaji wa muziki.


@lizerclassic wasipokupa heshima yako, wewe wape makaratasi ya kusaini wakati unafanya kazi zao na kuoitisha SIKIO la mwisho na asiyejua thamani ya kalamu juu ya karatasi mwambie aweke dole gumba kisha kazi ifanyike, hapo watakuheshimu muda wa maokoto.

NAKUPA MAUA NA MTI WAKE.#theblackgodfather" ameandika @babutale

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page