top of page

KISA BARIDI MWANAMKE WA KENYA AFARIKI SIKU 5 BAADA YA KUWASILI CANADA KUTAFUTA MAISHA MAZUR


Kifo cha kusikitisha cha Delphina Wambui Ngigi, mwanamke Mkenya mwenye umri wa miaka 46 kimeiacha familia yake katika majonzi.

Wambui aliaga dunia siku tano tu baada ya kuwasili nchini Canada ambapo alikwenda kwa ajili ya kutafuta fursa bora zaidi.

Alikuwa na nia ya kuungana na Wifi yake kisha waingie kutafuta kazi, lakini ndoto zake zilikatizwa na kifo wakati akisubiri kukamilisha mchakato wake wa kupata nyaraka mbalimbali



na vibali ukamilike.

Mwanamke mmoja anayeishi jijini Toronto aitwae Teresa Wanjiku amesema Wambui alidaiwa kufariki baada ya kukabiliwa na baridi kali.

"Alinipigia simu na kuniambia aliambiwa asubiri nje ambapo baridi ilikuwa kali nilimwambia asubiri kama alivyoelekezwa. Kwani Nisingeweza mkaribisha kwangu kwa sababu alilazimika kwenda kwenye makazi maalumu ya wakimbizi kwani alikuja kama mkimbizi na si mgeni wa kawaida” anaeleza Wanjiku.

Mwanadada huyu aliamua kwenda kusaka maisha Canada ili asadie familia yake baada ya kupoteza kazi na kumpoteza baba yake hivyo nia yake ilikuwa awasaidie watoto wake na yeye wawe na maisha mazuri lakini baridi kali iliyompiga akiwa nje anasubiri kuweka mambo sawa ilikatisha uhai wake.

Kwa sasa familia yake ndugu, jamaa na marafiki wanatafuta kuchangisha USD40,000 sawa na Tsh Milioni 102 ili kurudisha mwili wake Kenya ambapo hadi kufikia sasa Milioni 10.6 zimekusanywa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page