top of page
Radio on air

KISA KULIWA TSH MILIONI 1 NAAVIATOR MWALIMU AJINYONGA...

Mwalimu wa sekondari ya Wavulana ya Nyamira nchini Kenya, amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake.

Mwalimu huyo aliyetambulika kwa jina la Kevin Omwenga mwili wake ulipatikana ndani kwake jana Alhamisi Juni 7, 2024, huku ikidaiwa kuwa alipoteza Ksh50,000 sawa na TSh Milioni Moja kwenye kamari maarufu kama aviator au kindege.




Msaidizi wa chifu wa eneo hilo, Johnson Manyara amethibitisha kifo cha mwalimu huyo wa masomo ya kemia na hisabati.

Baadhi ya walimu walidai Omwenga alipenda sana mchezo wa kamari wa aviator na alikuwa na deni kubwa ambapo alikuwa amekopa pesa kutoka kwa wenzake, zinazodaiwa kufika Ksh50,000 (Sh1 milioni) ambazo huenda alipoteza kwenye kamari hiyo.

"Nimekusanya kutoka kwa wenzake kwamba alikopa pesa nyingi, lakini alipoteza nyingi akicheza mchezo wa aviator," Manyara amesema. Mkuu wa Shule, George Onkundi amesema marehemu alionekana karibu na shule hiyo Jumatano lakini hakuripoti kazini.

"Bado hakuwa ameajiriwa na TSC, lakini alikuwa akifundisha nasi chini ya BOM kwa miaka minne iliyopita. Hakuonyesha dalili yoyote ya msongo wa mawazo," amesema mkuu wa shule huyo.

Kulingana na mkuu wa shule, simu zilizopigwa katika simu ya Omwenga usiku wa Jumatano na Alhamisi asubuhi hazikupokelewa, na kusababisha baadhi ya walimu kumfuata kwake kumtazama.

Mkuu huyo amesema baada kufika kwake walibisha mlango bila kujibiwa, ndipo wakaamua kuchungulia dirishani na kuuona mwili wake ukiwa umening'inia.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page