Na VENANCE JOHN
Maafisa nchini Marekani wamesema wamepata kifaa cha kurekodi taarifa (data) na kinasa sauti cha ndege, kinachojulikana kama kisanduku cheusi, kutoka kwenye ndege ya American Airlines.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_62372ac8280a4441a7f8c40ff9493e8a~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_62372ac8280a4441a7f8c40ff9493e8a~mv2.jpeg)
Kisanduku cheusi kinaweza kusaidia kutoa vidokezo kuhusu kile ambacho huenda kilikosewa kwenye ndege au kilichopelekea kutokea kwa ajili. Kulingana na runinga ya CBS, vinasa sauti hivyo vitachanganuliwa katika maabara ya Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Uchukuzi, karibu na eneo la ajali.
Ndege ya abiria inayoendeshwa kibiashara ya America Airline iligongana na helikopita ya jeshi la Marekani ya Black Hawk na kuangukia mtoni. Ndege hiyo ilikuwa na abiria 60 na wafanyakaiz 4 na mpaka sasa taarifa zilizopo ni kuwa watu 67 wamefariki kutokana na ajili hiyo ikijumuisha wanajeshi waliokuwa kwenye helikopta.
Comments