top of page

KITUO KIFUATACHO KIMATAIFA




KITUO KIFUATACHO KIMATAIFA NI PACOME DAY DHIDI YA CR BELOUIZDAD JUMAMOSI FEB 24

Kutoka kwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe amefunguka haya

"Kuna nafasi kubwa ya Yanga SC kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa endapo tutashinda mchezo ujao dhidi ya CR Belouzidad, hakuna namna nyingine ya kufanya hivyo ni lazima mchezo huo tutapate alama tatu hizo, kwenye kundi letu kila timu inaonesha kuwa ina uwezo wa kufuzu kwa lugha rahisi kila mtu ni mbabe

Licha ya kuwa na ratiba ngumu, tutahitaji kucheza mechi nyingine zilizopo mbele yetu ili kujenga utimamu wa mwili wachezaji wetu kuelekea mchezo huo. hivyo hakuna sababu ya kudeka deka, mchezo wetu na Polisi Tanzania FC ipo pale pale Chamazi. Kule Morogoro tumewaonjesha kidogo sumu ambayo tumeandaa kwa ajili ya mwarabu."

"Tulianza na mtoko wa Max, Aziz Ki, Bacca na GSM, Mchezo wetu wa awali na CR Belouizidad wengi tulifurahishwa na namna ambavyo timu ilicheza lakini tukahuzunishwa na matokeo. Mchezo huu tunakwenda na agenda kadhaa, kushinda na kulipa deni la magoli matatu.

"Uongozi na benchi la ufundi tumekubaliana kama taasisi Jumamosi ikawe Pacome Day, ukisema Pacome Day mwisho unamalizia Kitaalamu zaidi, unaweza kupaka rangi kichwani au kwenye ndevu. Kama huwezi kupaka rangi basi unaweza kujichora chochote na wanawake wanaweza kupaka kucha rangi."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page