top of page

KOCHA BENCHIKA NA WASAIDIZI WAKE WOTE BYE BYE SIMBA SC

Taarifa kwa umma iliyotolewa na klabu ya Simba SC inaeleza kuwa Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba kati yetu na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake wawili Kamal Boujnane na Farid Zemit.




Mwalimu Benchikha ameomba kuvunja mkataba wake kutokana na matatizo ya kifamilia yanayomkabili nyumbani kwao Algeria.

Mwalimu Abdelhak Benchikha ameueleza uongozi wa Simba kuwa anauguliwa na Mkewe hivyo anahitaji muda kuwa karibu nae na kumuuguza. Kwa kuzinga- tia umuhimu wa jambo hilo Uongozi umeridhia ombi la Mwalimu Abdelhak Benchikha.

Uongozi wa klabu ya Simba unamshukuru Mwalimu Abdelhak Benchikha kwa kipindi chote alichotumikia ndani ya timu yetu na tunamtakia kila la heri na tunamuombea Mkewe apate afya njema.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page