top of page

KOREA KUSINI YA TENGENEZA ROBOTI AMBAYO HUSAIDIA WALIOPOOZA KUTEMBEA

Na VENANCE JOHN


Watafiti wa Korea Kusini wameunda roboti nyepesi inayoweza kuvaliwa ambayo inaweza kumsaidia mtu kutembea hata kama mtu huyo amepooza. Roboti hiyo hutumiwa kwa kuivaa na kujifungia kwao, ambapo humwezesha kutembea, na hata kupanda ngazi.


Timu ya Maabara ya Exoskeleton katika Taasisi ya Juu ya Sayansi na Teknolojia ya Korea (KAIST) imesema lengo lao ni kuunda roboti ambayo inaunganisha kikamilifu katika maisha ya kila siku ya watu wenye ulemavu au waliopooza hasa upande wa chini wa mwili.


Kim Seung-hwan, ambaye mwenyewe ni mlemavu wa miguu na sehemu ya timu ya KAIST, alionyesha mfano ambao ulimsaidia kutembea kwa kasi ya kilometa 3.2 ka saa (kph) na hata kupanda ngazi kwenda sakafu ya juu ya gorofa. "Roboti hii inaweza kunikaribia popote nilipo, hata ninapokaa kwenye kiti cha magurudumu, na kuvaliwa ili kunisaidia kusimama, ambayo ni moja ya sifa zake tofauti," Kim alisema.


Roboti hiyo inayojiendesha iliyopewa jina la, WalkON Suit F1, imeundwa kwa aluminiam na titanium ili kuwa na uzito wa kilo 50 na huendeshwa na injini 12 za kielektroniki ambazo huiga mizunguko ya viungo vya binadamu wakati wa kutembea.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page