top of page

KUANZA UZALISHAJI MKUBWA WA AIRPODI ZENYE KAMERA IFIKAPO 2026...

Na Nassor Nangi

Kulingana na ripoti mbalimbali ikiwemo jarida maarufu mtandaoni liitwalo Wealth, kampuni ya uzalishaji wa vifaa vya kielektroniki iitwayo Apple, ipo tayari kuanza utengenezaji wa AirPods (vifaa maalumu vya kusikulizia sauti masikioni) zenye kamera ndani yake ifikapo mwaka 2026.




AirPods hizo zinatarajiwa pia kuwa na kamera za infrared (IR), sawa na zile zinazotumika katika teknolojia ya Kitambulisho cha Uso cha Apple (Face ID), Kamera hizi zinaweza kuwezesha ufahamu ulioimarika kusaidia kutambua yaliyokuzunguka katika mazingira utakayokuwa ukiwa umevalia AirPods hizo.

Foxconn, msambazaji wa muda mrefu wa Apple, anaripotiwa kuwa katika nafasi ya kuwa msambazaji wa bidhaa kwa moduli hizi zenye kamera za IR.

AirPods hizi zilizo na kamera zinatarajiwa kutumika na vifaa vya kichwa vya Apple Vision Pro na uhalisia ulioboreshwa wa siku zijazo (AR) na bidhaa za uhalisia pepe (VR).

Kuhusu gharama za bidhaa hizo bado haijawekwa wazi rasmi mpaka sasa.

Unatamani kupata AirPods hizo?

Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page