top of page

KUNA MTU MMOJA HAPO KIKAO KIZIMA ANAONGEA SENTENSI 2 TU TULIPE TSH NGAPI & YANGA BINGWA

Kutoka kwa Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick amepost picha hii na kuandika ujumbe huu "Hii picha ina mtu mmoja yeye kwenye kikao kizima huwa anaongea sentensi mbili tu, " shilingi ngapi tulipe?" baada ya hapo kikao kikiisha anasema "Yanga bingwa" hana maneno



mengi.

Wananchi shoutout kwa Tajiri wa mpira GSM, Tumuombee dua huyu kiumbe ni wa ajabu sana, dirisha la usajili likifunguliwa mtafurahi sana.

Tutachukua kombe la ligi miaka 10, Eng. Hersi Said 09.04.2024."Ameongeza pia

Wazee wetu walisema ubingwa hauna raha kama haujamla mtani, msimu huu mtani kaliwa nje ndani yaani 5-1 & 2-1 hivo tutasherekea ubingwa wa 30 kwa kumla mtani goli 7-2.

Hongereni sana Wananchi, timu kubwa ujidhihirisha uwanjani! Until we meet again. Asanteni sana wazee wetu wa Yanga, pia samahani sana wanachi wa DSM kwa kuwaharibia ratiba ya mvua leo, itaendelea kesho

NB: Baada ya kichapo tunataka kujua timu ni ya Mwenyekiti au Rais" Simon

Kwa taarifa za uhakika saa 24 tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page