Na VENANCE JOHN
Waasi wa Houthi nchini Yemen wametishia kufanya mashambulizi kwa Israel ikiwa nchi hiyo haitaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki sita huko Gaza.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_2733b3b5a5924deaae56e5535d3453de~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_2733b3b5a5924deaae56e5535d3453de~mv2.jpeg)
Katika hotuba yake kwenye runinga jana usiku, kiongozi wa kundi hilo Abdul-Malik al-Houthi amesema mafanikio yaliyofikiwa katika mazungumzo kati ya Israel na Hamas ni maendeleo muhimu, na kwamba kundi hilo linafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa wanamgambo hao wako tayari kutoa msaada wa kijeshi kwa Wapalestina ikiwa kutashuhudiwa ukiukwaji au mashambulizi ya Israel. Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakikabiliana na Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja ili kudhihirisha uungwaji wao mkono kwa Wapalestina katika vita vya Gaza.
Comments