top of page

KUTANA NA KINYOZI ASIYE JULIKANA

Na VENANCE JOHN


Umewahi kufikiri kwamba unaweza kwenda saluni kwa kinyozi na ukanyolewa kisha usiweze kutambua sura ya aliyekunyoa?


Kwa majirani zetu Kenya, kaunti ya Mombasa kuna kinyozi ambaye ameamua kuwa mbunifu kwani huvaa kifunika uso (mask) muda wote awapo maeneo ya kazi hivyo huwezi kutambua sura yake.


Kinyozi huyo amejizolea umaarufu na sasa anaitwa kinyozi asiye julikana, na kifunika uso chake (mask) alikiagiza toka nje ya Kenya, na anaweza kukitumia kwa miaka mitano (5). Wengi wa wateja wake wanamsifia kwa huduma yake nzuri, kwani ananyoa vizuri.


Mdau wetu unaweza kutuambia, uko tayari kunyolewa na mtu aliyeficha sura yake?

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page