top of page

Kutoka kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa Staa wa Bongofleva

Harmonize amesema jumamosi ya Mei 25 mwaka huu 2024 anatarajia kuzindua albamu yake ya tano katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambayo ameipa jina la 'Muziki wa Samia' akiwa na lengo kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

Harmonize amesema album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko



kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmoja mmoja na sio album tena. Harmo amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku wa mialiko na hakutakuwa na viingilio "Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia"

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page