top of page

KWA HOFU WAKAZI WA GOMA WAWASALIMIA NA KUWAKARIBISHA KWA SHANGWE WAASI WA M23

Na VENANCE JOHN


Wakaazi wa jiji kubwa zaidi mashariki mwa DR Congo wa Goma walisalimiana na waasi wa M23 wakati wakiwasili katika jiji hilo. Katika baadhi ya maeneo ya Goma, kitovu cha shughuli za kibinadamu katika eneo lote, wakaazi walijipanga barabarani kuwashangilia na kuwapigia makofi wapiganaji hao wenye silaha kali.


"Karibu, karibu marafiki zetu," baadhi ya watu waliimba kwenye video moja ilikuwa inasambaa kwenye mitandao ya kijamii. Wakaazi wanne waliohojiwa na shirika la habari la Reuters, ambao waliomba kutotajwa majina yao kwa kuhofia kulipizwa kisasi, walisema kuwa makaribisho hayo yametokana na kujilinda na sio kwamba wanawapenda waasi hao.


"Tunajaribu kuwa wema kwa sababu kuna hofu. Kwa kuwa wao ni wahalifu, hatuwezi kutabiri tabia zao," alisema mkazi mmoja aliyepatikana kwa njia ya simu. Na kuongeza; "Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kuonyesha kwamba tuna furaha."


Waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda, kwa hofu hapo jana, wengine walisalia majumbani na wengine walitoka kushangilia katika kile walichokiita kuonyesho furaha. Wapiganaji wa M23 waliingia Goma, jiji ambalo liko kando ya ziwa ambapo jiji hilo lina watu wapatao milioni 2, Jumapili kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka 13 lilitekwa na kuwa chini ya kundi hilo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page