Na VENACE JOHN
Mke wa rais wa zamani Michelle Obama hatahudhuria kuapishwa kwa Donald Trump wiki ijayo. Taarifa hii imetolewa na ofisi yake hapo jana, bila hata hivyo kutoa maelezo ya uamuzi wake. Uamuzi wa kuacha kuhudhuria hafla ya kuapishwa rasmi kwa Trump ni kuvunja utamaduni wa sherehe hiyo, ambapo marais wa zamani na wake zao hushiriki.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_70e4b00e768d46ec993e5ca1e035890a~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_70e4b00e768d46ec993e5ca1e035890a~mv2.jpeg)
Michelle Obama pia hakuhudhuria ibada ya kumbukumbu wiki iliyopita ya Rais wa zamani Jimmy Carter lakini mume wake, Barack Obama alihudhuria ibada hiyo na aliketi karibu na Trump na kushiriki naye mazungumzo.
“Rais wa zamani Barack Obama amethibitishwa kuwa atahudhuria sherehe za 60 za kuapishwa. Lakini mke wake Michelle Obama hatahudhuria sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 20 mwezi huu wa Januari.
Pia rais wa zamani George W. Bush na Laura Bush watahudhuria uzinduzi huo, ofisi yake imesema. Michelle Obama amekuwa akizungumza waziwazi kuhusu chuki yake dhidi ya Trump, ambaye amemshutumu kwa kuweka usalama wa familia yake hatarini kupitia matamshi yake.
Comments