top of page

KWA UONGOZI WA RAIS SAMIA IPO SIKU KOMBE LA CAF LITAKUJA TANZANIA- PROPHET KABOZYANGILI

Kutoka kwa Prophet Kabozyangili ana ujumbe huu kuhusiana na timu za Simba na Yanga kunako anga za Kimataifa

"Mwenye macho ameona, mwenye masikio amesikia, Afrika nzima imesimama na dunia imejua kuwa Tanzania kwenye suala michezo hususani wa mpira wa miguu ni tishio na kabla ya mwaka 2030 kufika ndani ya uongozi wa malkia wa Tanzania huyu, kuanzia 2025 na 2026 naamini kombe hili la Klabu Bingwa Afrika huende litakuja Tanzania zaidi ya mara mbili mfululizo




nadhani mmeona mechi ya jana Young Africans SC kilichotokea wamenyimwa haki yao hivyo wangepita huenda wangefika fainali na kombe hili lingekuja kwenye mikono ya Watanzania. Historia kama hizi hazikuwahi kutokea kwa Tanzania kuisimamisha Afrika na dunia kwa ubora wa Timu zetu za Yanga SC na Simba SC makubwa yote haya yameletwa na uchapakazi na ueledi wa malkia wetu @samia suluhu hassan, narudia tena kusema Mungu bariki ndani ya uongozi huu wa mama kuanzia 2025 hadi 2030 kombe hili la Klabu Bingwa Afrika litakuja Tanzania zaidi ya mara mbili mfululizo, hivyo tumpongeze rais wetu kwa kutupenda Watanzania wote pia tuungane wote kwa umoja wetu kuhakikisha 2025 mapema sana anapita bila kupingwa, miaka 3 tumeona tunataka kuona zaidi,mungu ibariki Tanzania mbariki Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan muongezee afya na umri ili atupe ulichomjalia mlinde kwa kila namna Watanzania bado tunamwitaji Ameni." Prophet Kabozyangili.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page