top of page

LATRA YAIKALIA KOONI NEWFORCE NA SAULI...




Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewaita na kufanya kikao na wasafirishaji wa Kampuni ya Newforce Enterprisess na Sauli kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu, mawili yanayomilikiwa na kampuni hizi kila moja na gari moja la mizigo lenye usajili wa nchi jirani. Ajali hiyo ilitokea eneo la mashamba ya mpunga, Kibaha mkoani Pwani, Machi 28,2024.

Kikao hicho kimefanyika ofisi za LATRA Dar es salaam na kuhudhuriwa na Bw. Johansen Kahatano, Kaimu Mkurugenzi Mkuu LATRA, ACP Michael Deleli, Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Tanzania na wawakilishi wa Makampuni hayo.

Akizungmza na wanahabari baada ya kikao hicho Bw. Johansen Kahatano, Kaimu Mkurugenzi Mkuu LATRA amesema kuwa baada ya Mamlaka kusikiliza pande zote kwenye kikao hicho, wasafirishaji hao wamepewa siku 7 kutoa maelezo kwa maandishi juu ya tukio hilo na hatua watakazo chukua.

Naye ACP Michael Deleli, Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Tanzania amewataka wasafirishaji kwa ujumla kutambua wajibu wao na kuwasimamia madereva na wahudumu ili kuhakikisha safari zinakuwa salama na bora.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page