Na VENANCE JOHN
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Bw. Godbless Lema amesema kuwa, ikiwa uchaguzi wa mwenyekiti ndani ya chama hicho utafanyika kwa uhuru, uwazi na haki basi Mwenyekiti wa wa sasa anayetetea kiti chake, Freeman Mbowe hawezi kushinda.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_76821061800e4250bf063054b73fa925~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_76821061800e4250bf063054b73fa925~mv2.jpeg)
Lema tayari ametangaza kumuunga mkono makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu kuwania nafasi ya mwenyekiti Taifa. Lema amesema wanachama wengi waliopo kwenye ngazi za maamuzi wanamuunga mkono Lissu wala sio Mbowe.
“Ninachowaambia ni kuwa kama uchaguzi utakuwa huru na haki, mwenyekiti hawezi kushinda take my word. Yaani mwenyekiti ana watu wachache sana wanaomuunga mkono,” amesema Lema. Godbless Lema ameyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi habari jijini Dar es Salaam.
Ikumbukwe kuwa Desemba 22, 2024, Mbowe akizungumza baada ya kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo, makao makuu ya chama Mikocheni aliziagiza mamlaka zinazosimamia uchaguzi wa chama hicho, kutenda haki ili ipatikane safu bora, yenye sifa na inayokubalika kuongoza.
Kommentare