top of page

LIGI YA MPIRA WA KIKAPU MAREKANI, MAMBO IKO HUKU

Na Ester Madeghe,


Ligi ya mpira wa kikapu imeendelea Usiku wa kuamkia Leo Tarehe 24/10/2024 kwa michezo mbalimbali kupigwa kwenye viwanja (Arena) tofauti pale Nchini Marekani. Indiana Pacerswameshinda Vikapu 115 kwa 109, Orlando Magic wamevuna vikapu 116 kwa 97 vya Miami Heat, wakati Cleverland Cavalier wakiwabugiza vikapu 136 kwa 106 vya Toronto Raptors.


Atlanta Hawks Wakishinda vikapu 120 kwa 116 vya Brooklyn Nets, Golden State Wariors Wakishinda 139 kwa 104 za Portland Trail Blazers, Milwaukee Bucks wakiibuka vikapu 124 _109 vya Philadephia 76ers.


Charlote Hornets wameshinda 110_105 vya Houston Rockets, New Orleans Pelican vikapu 123 kwa 111 vya Chicago Bulls, Memphis Grizlies Wakishinda 126 kwa 124 mbele ya Utah Jazz wakati Phoenix Suns wakishinda vikapu 116 kwa 113 vya LosAngeles Clippers.


Majira ya saa ya 8 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Washngton Wizards wanawaalika Boston Celtis, Saa 8:30 Usiku Dallas Mavericks wanamenyamana na San Antonio Spurs, Saa 11:00 Alfajiri Sacramento Kings wanamenyama na Minesota Timberwolves na Denver Nuggets dhidi ya Oklahoma City Thunder.


Ukanda wa mashariki timu tano za juu ni Boston Celtics, Orlando Magic, Indiana Pacers, Cleverland Cavaliers na Milwaukee Bucks huku Ukanda wa Magharibi timu tanoza juu ni Phoenix Suns, Golden State Warriors, LosAngeles Lakers, Memphis Grizlies na New Orleans Pelicans.


Mpaka Sasa Jayson Tatum wa Boston Celtics ana wastani wa Kukusanya point 37 kwa mchezo huku Anthony Davis wa Los Angeles Lakers ana wastani wa point 36. Je, Chama gani kutwaa NBA msimu huu? Funguka

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page