top of page

LULU ATIMIZA MIAKA 29...



Muigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu leo Aprili 16 ametimiza miaka 29 toka azaliwe mwaka 1995, Lulu alianza kujizolea umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 2000 akicheza uhusika wa mtoto kwenye maigizo mbalimbali ya Kundi la Kaole Sanaa na kisha baadae kucheza filamu mbalimbali.

Kupitia ukurasa wa mumewe ambaye ni Mfanyabiashara maarufu Majizzo amemuandikia ujumbe huu mkewe kipenzi akisherehekea birthday yake

"Kwanza tunamshukuru Mungu kwa zawadi kubwa alizotupatia, Imekuwa kawaida kila siku yake ya kusherehekea birthday ninakuwa ninapost jambo ambalo hamkuwahi kuliona yaani "Exclusive", Mwaka 2022 ilikuwa baraka kwenye nyumba yetu Bwana "G" alitamba kuwa Kaka baada ya kumpata Dada yake "G"

Leo katika siku ya kuzaliwa Mke wangu @elizabethmichaelofficial kwanza ninampongeza kwa kuwa Mama bora kwa watoto wetu na mke mwema kwangu.

Tuzidi kuombeana heri, Mungu awaajilie watoto wetu (wangu na wenu) kukua kwema, wawe watu hodari, wacha Mungu na wenye mafanikio makubwa.

Ahsante kwa kila kitu Mke wangu @elizabethmichelofficial" aliandika Majizzo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page