top of page

M/KITI WA KITONGOJI AUAWA KIKATILI KISA MKE WA MTU

M/KITI WA KITONGOJI AUAWA KIKATILI KISA MKE WA MTU

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Dudiye, Kijiji cha Dudiye, Kata ya Arri wilayani Babati, Manyara, Sadikiel Mlundi ameuawa kikatili kwa kukatwakatwa kwa kitu chenye ncha kali katika shamba la Chama cha Ushirika cha Rift Valley (RIVACU) akituhumiwa na mkazi wa kijiji hicho kuwa anajihusisha na uhusiano wa kimapenzi na mke wake.



Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Februari 23, 2024 katika Kitongoji cha Meras jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mtuhumiwa wa tukio hilo, Theophil Bakari ambaye ni fundi ujenzi.

Inaelezwa kwamba kwa muda mrefu, Theophil alikuwa akimtuhumu mwenyekiti huyo kutembea na mkewe na kumkanya mara kadhaa ambapo siku ya tukio, inaelezwa kuwa mtuhumiwa alichukua simu ya mke wake na kuanza kuwasiliana na marehemu kwa njia ya meseji akijifanya yeye ndiyo mwanamke huyo na kumuelekeza mahali pa kukutana.

Inazidi kuelezwa kuwa, bila kujua kwamba anaingizwa kwenye mtego, mwenyekiti huyo alielekea sehemu walipokubaliana kwenye meseji, ndipo akakutana na 'mbaya' wake ambaye alimshambulia kwa vitu vyenye ncha kali na kusababisha awe mahututi kabla ya baadaye kupoteza maisha.

Baada ya kutekeleza tukio hilo, inaelezwa kuwa Teophil alienda kujisalimisha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Dudiye na kueleza alichokifanya.

Akizungumza katika eneo la tukio, mke wa marehemu amesema alipigiwa simu kwa namba ngeni akitakiwa aongee na mumewe huku mtuhumiwa akijua ameshakamilisha dhamira yake.

Tukio hilo la mauaji ni la pili kutokea ndani ya wiki moja,

ambapo Februari 20, 2024, mtoto mwenye umri wa miaka 7,

aliuawa kikatili katika Kijiji cha Mapea, Kata ya Magugu

wilayani Babati.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page