Na VENANCE JOHN
Muungano wa makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiongozwa na M23 wametangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kibinadamu kuanzia leo Jumanne. Katika taarifa, makundi hayo yanayodaiwa kuungwa mkono na Rwanda wametaja sababu za kibinadamu za kusitisha mapigano, baada ya kuteka maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_3e604e4c5a4c43688f02949a6e8c1a6c~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_3e604e4c5a4c43688f02949a6e8c1a6c~mv2.jpeg)
Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 900 wameuawa na wengine 2,880 kujeruhiwa katika mapigano ya hivi majuzi karibu na Goma, jiji kubwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Congo DRC. Mataifa saba tajiri ulimwenguni yanayojulikana kama G7 na Umoja wa Ulaya (EU) yamelaani mashambulio hayo yakisema hiyo ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa DR Congo.
Muungano wa makundi ya waasi unaojulikana kama Muungano wa Mto Congo umeshutumu jeshi la Kongo (Congo River Alliance) kwa kuua watu wakitumia ndege kupiga mabomu katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi hao. Mpaka mashirika karibu yote ya misaada yamelazimika kusitisha usambazaji wa misaada kwa kuhofia usalama wao baada ya mashambulizi kuongeza zaidi.
Comments