top of page
Radio on air

MAANDAMANO YA KUPINGA MUSWADA WA FEDHA NCHINI KENYA YAGEUKA KUMTAKA RAIS RUTO AJIUZULU..

Na mwandishi wetu Venance John.

Maandamano yaliyogeuka kutoka kupinga muswada Wa fedha na kuwa ya kumtaka Rais Ruto kujiuzulu yametikisa miji mikubwa nchini Kenya, huku vijana waandamanaji wakieleza



kutoridhishwa na serikali ya Kenya Kwanza.

Leo saa 5:00 asubuhi, waandamanaji waliingia barabarani katika eneo la katikati mwa jiji la Nairobi wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo za kupinga serikali.

Katika baadhi ya miji ikiwemo jiji kuu la Nairobi Polisi wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali.

Katikati ya jiji biashara nyingi zimefungwa.

Waandamanaji pia wameingia katika mitaa ya miji mingine ikiwemo Mombasa na Kisumu.

Hata hivyo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema tangu maandamano ya kupinga muswada wenye utata wa fedha kuanza wiki mbili zilizopita watu 39 wameuawa na vikosi vya usalama.

Katika mahojiano ya hivi karibuni Rais William Ruto alisema Hana damu mikononi mwake huku akisema kuwa taarifa aliyonayo, ni watu 19 ambao wamefariki kutokana na maandamano hayo.

Licha ya kuamua kuutupilia mbali mapendekezo ya nyongeza ya ushuru, lakini maandamano yamebadilika na kuwa wito wa kujiuzulu na hasira juu ya ukatili wa polisi.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page