top of page
Radio on air

MACHACHE UNAYOTAKIWA KUJUA JUU YA UCHAGUZI WA AFRIKA KUSINI UNAOFANYIKA LEO..

Siku ya leo Jumatano ya 29 May, Taifa la Afrika Kusini limeanza rasmi kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kuchagua viongozi mbalimbali watakalolingoza Taifa hilo akiwemo rais kwa safari ya miaka 5 ijayo.

Huu unakuwa uchaguzi wa saba(7) kufanyika tangu 1994, ulipofanyika uchaguzi wa kwanza ulimuweka madarakani Hayati Nelson Mandela kupitia Chama Cha ANC aliyepata 62.5% ya viti 400 vya ubunge.

Baada ya miaka 30 ya utawala wa Chama Cha African National Congress(ANC) mwaka huu inategemewa kukabiliwa na upinzani mkali zaidi katika historia, ili kupata asilimia 50%, ili iweze



kutawala bunge ambapo mpaka sasa kabla ya kuanza uchaguzi ilionyesha kukubalika kwa 43% tu.

Mfumo wa kumpata rais nchini Africa Kusini hauruhusu wananchi moja kwa moja kumchagua rais bali, wanashiriki kufanya uchaguzi wa Wawakilishi wa viti 400, ambapo Chama kitakachopata viti 201 ambapo itakuwa ni zaidi ya 50% ya viti vyote kitakuwa kimeshinda uchaguzi na kumpata rais ili kuliongoza Taifa hilo

Africa Kusini ina jumla ya watu milioni 62, huku wapiga kura milioni 27.79 wakijiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi huo kulingana na tume ya uchaguzi ya Africa Kusini(IEC) na mtu mzima mwenye umri wa miaka 18 tu ndiye anayeruhusiwa kupiga kura.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika kwenye jumla ya majimbo 9 yanayounda Taifa hilo, huku kukiwa na takribani manispaa 257, jumla ya vituo vya kupigia kura 23,292, na rais atakayechaguliwa atahudumu kwa takribani miaka mitano.

Baadhi ya viongozi wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi huo ni pamoja na: Cyril Ramaphosa(miaka 71) ANC

Kulingana na kura za maoni zilizoendeshwa na chombo cha habari cha eNCA, Ramaphosa ambaye ndiye rais aliyeko madarakani akiwakilisha Chama tawala cha ANC anaonekana kukubalika kwa 43.4% huku akitarajiwa kushinda majimbo 7 kati ya 9 nchini humo.

Kwenye uchaguzi uliopita mwaka 2019 ANC ilikuwa na uwakilishi wa viti 230 bungeni sawa na 57.5% John Steenhuisen(miaka 48) DA

Anashika nafasi ya pili akiwa na 18.6% za kukubalika akiongoza Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance(DA).

Mpaka sasa DA inaonekana kwenda kulitwaa jimbo la Western Cape, ambako linapatikana jiji la Cape Town, ambapo mwaka 2019, DA ilishinda 55.45% ikishinda uchaguzi ndani ya jimbo hilo na walifanikiwa kuwa na ushindi wa viti 84 vya uwakilishi bungeni sawa na 21%.

Jacob Zuma(miaka 82) MK

Rais wa zamani wa Africa Kusini na kiongozi wa zamani wa ANC, amerudi kwa mara nyingine na Chama chake kipya cha uMkhonto we Sizwe(MK) ikiwa na maana ya "Mkuki wa Taifa" huku akionekana kukubalika kwa 14.1%

Mpaka sasa anaonekana kukubalika zaidi katika jimbo la Kwazulu Natal.

Julius Malema(miaka 43) EFF

Anakamalisha top 4 akionekana kukubalika kwa 11.4% kupitia Chama chake Cha Economic Freedom Fighters(EFF) ambapo uchaguzi uliopita alikuwa na viti 44 vya uwakilishi bungeni sawa na 11%.

Mshirika wa zamani wa Jacob Zuma ambaye alifukuzwa na Chama Cha ANC mwaka 2012 baada ya kutofautiana na Zuma na kuamua kuanzisha Chama chake cha EFF mwaka 2013.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page