top of page

MAHAKAMA KENYA YAPIGA MARUFUKU POLISI KUTUMIA MAGARI YASIYO NA NAMBA ZA USAJILI, WATAKIWA PIA KUTOFICHA UTAMBULISHO WAO

Na VENANCE JOHN


Mahakama nchini Kenya imeiamuru huduma ya polisi kwamba polisi wanatakiwa kuonesha utambulisho wao ikiwa ni Namba ya askari au sare yenye jina ili kuhakikisha uwajibikaji unafanyika pale watakapo vunja sheria hasa wanapokuwa wanatuliza maandamano.


Amri hiyo imetolewa na mahakama kuu ikimwelekeza Insipekta Jenerali wa polisi kuhakikisha kwamba maafisa wa polisi hawafichi utambulisho wao wa sura pale wanapopelekwa kutuliza maandamano.


Polisi pia wameamriwa kuvaa sare zenye majina yao na namba ya polisi husika kwenye sare yake pale anapokuwa kazini. Sambamba na hayo, mahakama hiyo pia imepiga marufuku polisi kukamata watu kwa kutumia gari ambazo hazina namba ya usajili (plate number).


Amri hiyo imetoka baada ya chama cha wanasheria wa Kenya LSK kupeleka shauri mahakamani kwa hati ya dharura kikidai kwamba polisi na maafisa wengine wamekuwa wakitishia uwajibikaji kwa huduma ya polisi ya taifa hilo.


Mahakama imesema polisi waliovaa sare zenye majina yanayoonekana, au namba inayooneka, bila polisi hao kuficha nyuso zao, hao ndiyo watakaopaswa kupelekwa kuwalinda waandamanaji watakaokuwa wanatekeleza haki yao ya kikatiba.


Kwa mjibu wa rais wa LSK, Faith Odhibo, amesema maafisa wa polisi ambao wamekuwa wakiwadhuru waandamanaji ambao wanakuwa wanatekeleza haki yao ya kikatiba, polisi hao wanatakiwa kuwajibishwa.

Коментари


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page