Na VENANCE JOHN
Mahakama ya Uganda imeiamuru serikali nchini humo kulipa hadi shilingi milioni 10 za Uganda (dola 2,740) kwa kila mwathiriwa vita vilivyoendeshwa na kundi Lord's Resistance Army LRA chini ya kamanda Thomas Kwoyelo.

Thomas Kwoyelo ni mwanachama wa kwanza mkuu wa kundi la waasi kuhukumiwa na mahakama ya Uganda. Mwezi Oktoba, Kwoyelo, kamanda wa ngazi ya kati katika LRA, alihukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa uhalifu wa kivita ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, utumwa, utesaji na utekaji nyara.
Kulingana na uamuzi wa mahakama, Kwoyelo alipatikana kuwa hawezi kulipa fidia yoyote kwa waathiriwa kutokana na hali yake ya umaskini, na hivyo kusababisha mahakama kuamuru serikali kubeba gharama hiyo. Jeshi la Uganda lilimkamata Kwoyelo mwaka 2009 kaskazini mashariki mwa Kongo na kesi yake ikaingia katika mfumo wa mahakama ya Uganda hadi kuhukumiwa kwake mwezi Agosti.
Comments