top of page

MAHAKAMA YA ULAYA YASEMA SHERIA ZA FIFA ZA UHAMISHO WA WACHEZAJI ZINAKIUKA SHERIA ZA ULAYA, FIFA YAKUBALI

Na VENANCE JOHN


Mahakama kuu ya Umoja wa Ulaya imesema leo imesema kuwa baadhi ya sheria za FIFA kuhusu uhamisho wa wachezaji zinakwenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya na kanuni za kuhama timu kwa uhuru. Uamuzi huo unaweza kufungua milango kwa wachezaji kupata klabu mpya kwa urahisi zaidi baada ya mikataba yao kukatishwa.


Kanuni za FIFA kuhusu hadhi na uhamisho wa wachezaji (RSTP) zinasema mchezaji anayekatisha mkataba kabla ya muda wake bila sababu za msingi atawajibika kulipa fidia kwa klabu, na pale mchezaji anapojiunga na klabu mpya, basi yeye na klabu yake watawajibika kwa pamoja kulipa malipo ya fidia.


Mahakama ya haki ya Umoja wa Ulaya (CJEU), imetoa uamuzi huo baada ya kesi ya mchezaji wa zamani wa Ufaransa, Lassana Diarra aliyefungua madai dhidi ya klabu ya Lokomotiv Moscow ya Urusi.


Mwaka 2014 Diarra aliondoka klabu ya Lokomotiv Moscow baada tu ya mwaka mmoja akiwa na mkataba wa miaka minne ambapo klabu hiyo ilipeleka suala hilo kwenye Chama cha Kusuluhisha Migogoro cha FIFA kwa madai kuwa alikiuka kanuni wakati mkataba wake ulipositishwa baada ya mchezaji huyo kuamua kuondoka bila sababu za msingi baada ya kukatwa malipo.


Diarra alipokea ofa ya kujiunga na klabu ya Charleroi ya Ubelgiji lakini klabu hiyo iligoma baada ya FIFA kukataa kusaini hati ya uhamisho wa Kimataifa (ITC), na kuzuia mchezaji huyo kusajiliwa na shirikisho la Ubelgiji.


Mwaka 2015, FIFA iliamuru, Lassana Diarra kulipa Yuro milioni 10 sawa na dola milioni 11.05 kama fidia kwa klabu ya Lokomotiv, na kumfanya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea, Arsenal na Real Madrid kushtaki bodi ya FIFA na shiriko la mpira la Ubelgiji na kudai fidia mbele ya mahakama hiyo ya Umoja wa Ulaya.


Mhakama hiyo imesema kuwa tabia hizi hazikuwa halali, na uamuzi huo unatarajiwa kusababisha FIFA kurekebisha kanuni zake za uhamisho. Mahakama hiyo imesema sheria hizo zikizingatiwa, ni kama vile kuzuia uhamisho wa kimataifa wa wachezaji. Kulingana na uamuzi wa CJEU, pia ni kinyume cha sheria kukataa kutia saini ITC.


"Sheria zinazozungumziwa ni kama vile kuzuia uhuru wa kuhama kwa wanasoka wa kulipwa wanaotaka kuendeleza shughuli zao kwa kwenda kufanya kazi katika klabu mpya," imesema CJEU yenye makao yake nchini Luxembourg. Uamuzi wa CJEU pia unaweza kusababisha wachezaji wengine wa kulipwa walioathiriwa na kanuni za FIFA kama vile Lassana Diarra pia kutafuta fidia.


"Wachezaji wote wa kulipwa wameathiriwa na sheria hizi haramu zinazotumika tangu 2001 na kwa hivyo sasa wanaweza kutafuta fidia kwa hasara zao," mawakili wa Diarra Bw. Jean-Louis Dupont na Martin Hissel wamesema katika taarifa yao. Dupont ameongeza kuwa mfumo mzima wa uhamisho utabadilika kulingana na uamuzi wa mahakama.


FIFA imesema imeridhika na maamuzi dhidi ya uhalali wa kanuni muhimu za mfumo wa uhamisho katika uamuzi wa leo. “FIFA itachambua uamuzi huo kwa uratibu na wadau wengine kabla ya kutoa maoni zaidi,” shirikisho hilo la soka limesema.


"Kwa niaba ya chama cha wachezaji wa kulipwa duniani kote FIFPRO, chama hicho kimekaribisha maaamuzi ya mahakama hiyo David Terrier, rais wa FIFPRO kanda ya Ulaya, amesema walikuwa na furaha kwa Lassana Diarra lakini akasema kwamba Diarra sio mwathirika pekee

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page