top of page

MAHAKAMA YAMWONDOA MADARAKANI WAZIRI MKUU WA THAILAND KWA KOSA LA MAADILI

Na VENANCE JOHN


Mahakama ya Katiba nchini Thailand imemwondoa madarakani waziri mkuu wa nchi hiyo Srettha Thavisin hii tarehe 14, Agost 2024, kwa kukosa maadili kwani alimteua aliyewahi kufungwa jela kuwa waziri.


Srettha ameondolewa madarakani akiwa hajamaliza hata mwaka mmoja madarakani. Kufuatia umuzi huo wa mahakama, bunge litakaa siku ya ijumaa, kumchagua waziri mkuu mpya.


Srettha ambaye ni tajiri mkubwa wa mali hasa zisizohamishika (real estates) ni waziri mkuu wa 16 kuondolewa madarakani na mahakama ya katiba huku wajuzi wa mambo wakisema mahakama hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha kuleta migogoro mingi ya kisiasa nchini humo.


Nchi hiyo imekuwa kwa karibu miongo miwili (karibu miaka 20) ikikumbwa na mapinduzi ya kijeshi na wakati mwingine hukumu za mahakama ambazo zimekuwa zikiziondoa mamlakani serikali nyingi na vyama vingi vya siasa madarakani.


Srettha amekana kufanya makosa ya kumteua kwenye baraza Pichit Chuenban ambaye aliwahi kuwa mwanasheria wa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra.


Pichit Chuenban alifungwa mwaka 2008 kwa kosa la kudharau mahakama baada ya kutuhumiwa kuwa alijaribu kuwahonga wafanyakazi wa mahakama kosa ambalo hata hivyo halikuthibitishwa.


Chama cha waziri mkuu huyo aliyeondolewa cha Pheu Thai Party ambacho kiliungana na vyama vingine kuunda serikali, leo kimesema kwamba kesho kitakuwa na mkutano wa dharura ili kumchagua mtu anayeweza kuwa mgombea wa uwaziri mkuu katika kikao cha Ijumaa cha bunge kitakachokuwa na kazi ya kupiga kura ya kumchagua waziri mkuu mpya.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page