top of page

MAKALLA ACHUKUA NAFASI YA PAUL MAKONDA CCM..



Kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimemteua Amos Makalla kuwa wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

Makalla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kabla ya uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo aliondolewa katika nafasi hiyo.

Anachukua nafasi ambayo ilikuwa wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia Paul Makonda kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kikao hicho maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kimefanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page