top of page

MAKONDA ATULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:


1) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu



(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe. Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Anachukua nafasi ya Mhe. John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page