Na VENANCE JOHN
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameviagiza vikosi vya jeshi lake vinavyohudumu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanza kujiandaa kuwaondoa wanajeshi wake.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_8f5949f9788643fab4399c6d9d21f021~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_8f5949f9788643fab4399c6d9d21f021~mv2.jpeg)
Wanajeshi wa Malawi ni sehemu ya kikosi cha wanajeshi kutoka jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) waliotumwa nchini Kongo kuisaidia kupambana na waasi wenye silaha. Rais Chakwera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Malawi (MDF) kuanza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi wa Malawi.
Muungano wa waasi, unaojumuisha wapiganaji wa M23, ulitangaza kusitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu kuanzia siku ya Jumanne lakini taarifa za leo zinaeleza kuwa tayari mapigano yameanza tena katika mkoa jirani wa Kivu Kusini.
Na duru za kuaminika zinasema kuwa waasi wa M23 wamechukuwa udhibiti wa mji wa uchimbaji madini wa Nyabibwe, karibu kilomita 100 kutoka Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini
Comments