top of page
Radio on air

MAMA ADAIWA KUMTEKA MWANAE ILI BABA MTOTO ATOE TSH MILIONI 2O

Jeshi la Polisi Nchini linawashilikilia Watu watatu akiwemo Mama mzazi wa Mtoto kwa tuhuma za kuhusika kupanga njama za kumteka Mtoto wake wa kike mwenye umri miaka mitano ambae ni Mwanafunzi wa Shule ya awali iliyopo Jijini Mbeya ili wapate pesa kutoka kwa Baba mzazi wa Mtoto. Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mama mzazi wa Mtoto huyo Agnes Jacob



Mwalubuhi, Winfred Martin Komba na Hamida Gaudence Njuu ambapo Polisi wamesema baada ya kuripotiwa kwa taarifa za Mtoto kupotea Watu wasiojulikana walipiga simu kwa Baba mzazi wa Mtoto huyo, Layson Mkongwi na kumtaarifu kuwa hatompata Mtoto wake hadi pale atakapotuma Tsh. milioni 20. Akiongea leo May 24,2024, Msemaji wa Polisi Nchini David Misime amesema tarifa za kupotea Mtoto huyo ziliripotiwa May 15,2024 ambapo Polisi walianza ufuatiliaji kwa kina ili kufanikisha upatikanaji wa Mtoto huyo "Jana usiku wa saa nne kamili alikamatwa Winfred Martni komba (36) Mkazi wa vinguguti Jijini Dar es salaam ambaye ndiye aliyekuwa akipiga simu kwa Baba mzazi wa Mtoto akimtisha asipotuma milioni 20 hatampata Mtoto wake" "Baada kukamatwa Mtuhumiwa huyo alieleza ukweli kuwa walikula njama na Mama mzazi wa Mtoto huyo aliyemtaja

Agnes Jacob Mwalubuhi Mkazi wa Isyesye Jijini Mbeya ili kuweza kujipatia fedha kutoka kwa Baba mzazi huyo na kusema Mama huyo alimfahamu wakati wakiishi pamoja katika nyumba za kupanga eneo la Forest ya zamani Mbeya na kwamba baada ya kupanga njama hizo alifanikiwa kumchukua Mtoto huyo May, 15,2024 na kwenda kumficha kwa Rafiki yake aliyemtaja kwa jina Hamida Gaudence njuu

ambako Mtoto huyo alikutwa"

"Jeshi la polisi limechukua muda mrefu kumpata Mtoto huyo

kutokana na kila ambalo Polisi walikuwa wakipanga walikuwa wakimshirikisha Mama mzazi wa Mtoto wakidhani anauchungu na Mtoto wake kumbe yeye ndie alikuwa anapeleka taarifa kwa Mtuhumiwa mwenzake hivyo kumfanya aendelee kukimbiakimbia na kujificha.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page