top of page

MAMLAKA ZA UFARANSA ZAAPA KUFUKUZA WAHAMIAJI KUTOKA DRC KONGO.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa ameamuru mamlaka za Ufaransa ya Mayotte kupanga safari za ndege za kuwafukuza wahamiaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa madai ya nchi hiyo kuwa katika wakati wa kujaribu kudhibiti uhamiaji haramu kwenye kisiwa cha Mayotte karibu na pwani ya mashariki mwa Afrika.


Waziri mpya wa Ufaransa Bruno Retailleau amenukuliwa akiliambia bunge la Ufaransa "nataka kurejesha utulivu nchini Ufaransa", huku akitoa amri kwa mkuu wa jeshi la polisi wa Mayotte kuwa, anapaswa kupanga safari za ndege ili kuwasindikiza wahamiaji haramu kurudi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.


Washirika wanaomuunga mkono waziri huyo mpya wa mambo ya ndani wamesema kuwa, mpaka sasa safari tatu zimepangwa ili kusaidia vituo ambavyo vilikuwa kuzuizini. Kadhalika, licha ya hatua hiyo inayochukuliwa na mamlaka ya Ufaransa, lakini bado ushirikiano wa mamlaka katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo juu ya suala hilo umekuwa mzuri.


Kila mwaka maelfu ya watu kutoka visiwa jirani vya Comoro, na bara la Afrika huingia kwa siri katika kisiwa cha Mayotte, hali inayopelekea idadi ya wahamiaji kuongezeka hadi kufikia 320,000 katika kisiwa cha Mayotte.


Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page