Fahamu kuwa siku ya leo Machi 15 nyota wa Bongofleva Harmonize kutoka pale Konde Gang anatimiza umri wa miaka 30 ambapo ameutumia ukurasa wake wa Instagram kutoa ujumbe ambao ndani yake ameahidi kuwa mtu mpya asiye na ugomvi na msanii yoyote, katika sanaa yake ya muziki, akitolea mfano utofauti wake na Diamond Platnumz, kuwa hivi sasa watazika

tofauti zao na amani itatawala kati yao.
"Turn to 30 years of my life!! I just wanna thank everyone for supporting my music journey 8 years in the game and still number one, usitegemee kuniona nikifanya the same, nimechagua kuyakataa mabaya na kuyaendeleza mema. Naamini sikuzaliwa kuja kushindana wala kugombana. Mapenzi ya watu wote yamefanya tuwe na Number One Record Label @Kondegang kama YouTube na mitandao mingine yote inavyo onyesha" - Harmonize
"Wakati huu moyo wangu umejawa na furaha sana najiona namuona KONDE BOY MPYA mwenye miaka (30) hagombani, hana kinyongo na yeyote, anayemtanguliza MUNGU.
Nimeona baadhi ya watu wakisema amani itapunguza utamu wa game. Mawazo yangu yanapingana na hilo maana chuki zimekaa miaka kibao na hatujafikia kufanya makubwa wanayo fanya wenzetu Nigeria & South African, ifike mahala tuujaribishe upendo tuone nguvu yake"- amefunguka Harmonize.
Comments