top of page

MANYOYA YA NDEGE YAKUTWA KWENYE INJINI ZA NDEGE YA JEJU AIR ILIYOPATA AJALI

Na VENANCE JOHN


Wachunguzi wamesema wamepata ushahidi wa manyoya ya ndege kwenye ndege ya abiria iliyoanguka nchini Korea Kusini mwezi Disemba na kuua watu 179. Manyoya na madoa ya damu kwenye injini zote mbili za ndege ya Jeju Air yalitoka kwa ndege aina ya Baikal teal, aina ya bata wanaohama ambao huwa katika makundi makubwa. Hii ni kulingana na ripoti ya uchunguzi wa awali iliyochapishwa leo Jumatatu.


Uchunguzi kuhusu ajali hiyo mbaya zaidi katika ardhi ya Korea Kusini sasa utazingatia jukumu la shambulio la ndege na muundo wa zege uliokuwa mwishoni mwa njia ya kuruka na kutua, ambayo ndege ilianguka.


Injini za Boeing 737-800 zitavunjwa na muundo wa saruji utachunguzwa zaidi, ripoti hiyo ilisema. Ndege ya Jeju Air ilipaa kutoka Bangkok asubuhi ya tarehe 29 Disemba na ilikuwa ikiruka hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan kusini-magharibi mwa nchi ya Korea Kusini.


Saa 08:59, rubani aliripoti kwamba ndege hiyo ilimgonga ndege na kutangaza ishara ya dharura na hatari (mayday). Kisha rubani akaomba ruhusa ya kutua kutoka upande mwingine, ambapo ilitua kwa tumbo bila vifaa magurudumu yake ya kutua kutokeza. Ilivuka barabara ya kurukia ndege na kulipuka baada ya kugonga zege iliyokuwa mwisho wa uwanja.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page